Leo
Asubuhi, kila mtu anaona siku yake
Mahakama za leo na kesho, tarehe za kuwasilisha zinazokaribia, kazi zilizochelewa na malipo yanayosubiri kuthibitishwa. Mbia anaona ofisi nzima; wakili anaona kesi zake.

Kwa ofisi za mawakili Tanzania
Roote Legal inaweka kesi, diary ya mahakama, hati, rasimu, ankara na wateja wa ofisi yako mahali pamoja. Kila wakili anafungua faili analoruhusiwa, ofisini au mahakamani, kwenye kompyuta au simu.
Kiswahili na Kiingereza. Imejengwa Dar es Salaam na Roote Technologies.

Roote Legal inaweka faili kwenye mfumo mmoja wa ofisi. Mbia anaamua nani anaona nini: timu ya kesi tu, au ofisi nzima ili mawakili wadogo wajifunze kutoka kwa kazi ya wakubwa.
Mfumo wa ofisi
Leo
Mahakama za leo na kesho, tarehe za kuwasilisha zinazokaribia, kazi zilizochelewa na malipo yanayosubiri kuthibitishwa. Mbia anaona ofisi nzima; wakili anaona kesi zake.

Faili la kesi
Wahusika, mahakama, jaji, namba ya kesi, historia ya kila hatua, hati kwa makundi, maelezo, mjadala wa timu na ujumbe kwa mteja. Kila badiliko linaandikwa kwenye kumbukumbu.

Diary ya mahakama
Kutajwa, usikilizaji, uamuzi na mwisho wa kuwasilisha. Vikumbusho vinatumwa siku moja kabla na asubuhi ya siku hiyo, kwa wakili na katibu.

Kuandaa hati
Hati ya madai, barua ya madai, mkataba, kiapo: majina ya mteja na kesi yanajazwa yenyewe. Matoleo yanahifadhiwa, na mteja anaweza kusaini kwenye simu.

Fedha
Ankara kwa kesi, malipo kwa M-Pesa na benki, madeni kwa umri wake, na fedha za wateja zilizotunzwa kando kwenye akaunti ya amana.

Ndani ya ofisi
Wakili anaona kesi alizopewa tu. Wakili kiongozi au mbia akiruhusu, kesi inafunguliwa kwa ofisi nzima ili mawakili wadogo wajifunze. Ofisi moja haiunganishwi na nyingine kamwe.

Tovuti ya ofisi
Kwa jina la ofisi, picha zake, mawakili wake na maeneo yake ya sheria. Fomu ya mawasiliano inaingia moja kwa moja kwenye mfumo, na wateja wanaingia kwenye portal yao kupitia tovuti hiyo hiyo. Chagua moja ya mitindo mitatu.
Programu ya simu
Programu ya Android na iPhone inaonyesha kesi za siku, faili zima la kesi, diary na ujumbe. Hati zilizofunguliwa zinabaki kwenye simu hata mtandao ukikatika. Piga picha ya amri ya mahakama na iingie kwenye faili mara moja.
Simu ya Android itauliza ruhusa ya kusakinisha programu kutoka nje ya Play Store. Ingia na akaunti ya ofisi yako, au chagua "Jaribu ofisi ya mfano".
Usalama na siri ya mteja
Bei
Hatuhesabu watu. Kila mtu wa ofisi yako, na kila mteja kwenye portal, amejumuishwa. Bei inafuata nafasi ya kuhifadhi hati mnayohitaji.
Ada ya kuanzisha mara moja, kisha ada ya mwezi. Mkataba wa mwaka mmoja.
Inajumuisha tovuti ya ofisi, kuingiza hadi mafaili 100 yaliyopo, na mafunzo ya timu ofisini kwenu.
| Kiwango | Hifadhi | Kwa mwezi |
|---|---|---|
| EssentialOfisi ya mawakili 1 hadi 5 | 25 GB | TSh 150,000 |
| FirmOfisi ya kati yenye mafaili mengi | 100 GB | TSh 280,000 |
| ChambersOfisi kubwa na zenye matawi | 300 GB | TSh 480,000 |
| Kwenye hosting yenuHifadhi ni ya hosting yenu | Yenu | TSh 120,000 |
Kwenye hosting ya Roote, nafasi ikijaa mnaongeza GB 50 kwa TSh 25,000 kwa mwezi.
Mfumo unakuwa wenu, kwenye hosting yenu. Hifadhi inategemea hosting mliyonayo.
Matengenezo na masasisho ya mwaka, hiari: TSh 1,800,000.
Bei zote ni kwa shilingi za Tanzania. Malipo kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au benki. Jaribu siku 14 bure kabla ya kuamua.
Hapana. Anza na kesi zinazoendelea na tarehe zijazo; ongeza za zamani taratibu. Unaweza kupiga picha hati kwa simu moja kwa moja kwenye faili la kesi.
Kwenye seva salama zenye nakala kila usiku, au kwenye hosting yenu mkinunua mfumo. Ni watu wa ofisi yenu wenye ruhusa tu wanaoona kesi na hati. Wafanyakazi wa Roote wanaona akaunti na malipo, si mafaili yenu.
Hapana. Kila ofisi imetengwa kabisa; hakuna kiungo kati ya ofisi. Ndani ya ofisi, wakili anaona kesi zake tu, mpaka wakili kiongozi au mbia afungue kesi kwa ofisi nzima.
Ndiyo. Kwenye kivinjari cha simu yoyote na kwenye programu ya Android na iPhone, yenye vikumbusho vya mahakama.
Ni saini ya kielektroniki ya kawaida chini ya Sheria ya Miamala ya Kielektroniki (2015): ushahidi mzuri wa makubaliano. Hati ambazo sheria inataka saini ya mkono au kamishna wa viapo bado zinahitaji hivyo.
Ndiyo. Ni msaidizi wa kuokoa muda: kila jibu lina onyo na mnapaswa kuhakiki nukuu kabla ya kuzitumia. Uamuzi wa kisheria ni wenu.
Mnaweza kupakua kesi, ankara na kumbukumbu kwa CSV na hati zenu wakati wowote. Usajili ukiisha, bado mnaweza kusoma kila kitu.

Fungua ofisi yenu sasa, au tuombe tuje tuwaonyeshe na kuweka kesi zenu za kwanza pamoja nanyi.